Mafanikio ya Isaya ni makubwa. Kutokana na mahubiri yake na ushauri wa kiroho maelfu ya watu wametafuta na kupata ubatizo katika Kanisa la Kiinjili la Tanzania. Pia wamekubali mabadiliko mengi katika hali ya maisha yao. Kitabu hiki kimeandikwa ili sisi na kizazi kijacho tuwe na kumbukumbu ya haya yaliyochangia kwa sehemu kubwa kuwafanya Wamasai kuuongokea Ukristo. Lengo lingine ni kuwasaidia wachungaji, wainjilisti na mkristo yeyote yule kuona nuru katika giza la maswali mazito. Katika mafundisho yake, Isaya hugusa maswali yanayohusu dini, mila na desturi za Wamasai. Je, mafundisho yake Isaya ni halali? Au anachanganya mambo yasiokwen- da pamoja? Kwanza tunasikia jinsi alivyoitwa na Mungu juu ya mlima pale Kenya. Halafu tunasoma moja ya mahubiri ya Isaya. Na baadaye tunamfuata katika njia yake ndefu ya kupata ubatizo. Halafu tutaangalia huduma yake: Mhubiri Isaya na ujumbe wake, mpatanishi na mbinu zake, marafiki zake Joshua na Isaaka. Tutaangalia kazi yake katika Tanzania na tutasikiliza wenye hoja zao Kenya wasemavyo. Pia tutajaribu kujibu maswali: Je, Isaya Ole Ntokoti ni Oloiboni bado? Au ni mtu mwenye wito maalum wa Mungu kama nabii?
Jina Lako Ni Mpatanishi – Maisha Na Kazi Ya Isaya Orishi Olentokoti
Autor*in
Scheuerl, Stefan
ISBN: 978–3‑87214–909‑1
Auflage: 1
Erscheinungsdatum: 28.04.2014
Seiten: ca 236
Format (in cm): 21,0 x 14,8 cm
Gewicht (in g): 335
Produktform: Buch
Reiheninfo: Makumira Publication
Produktsprache: Swahili
Bewertungen
Es gibt noch keine Bewertungen.